3,000 For Sale
Ad Details
-
Ad ID: 13689
-
Added: 9th May 2021
-
Sale Price: 3,000
-
Location: Tanzania
-
State: NunuaUza.com
-
Phone: 0677775000
-
Views: 476
Description
KEKI/MKATE WA SEMBE (CORN BREAD)
Mahitaji:
*Unga wa sembe glass 1
*Unga wa ngano glass 1
*Mayai 4
*Maziwa fresh/ tui la nazi glass 1
*Sukari glass 1
*Mafuta nusu glass
*Baking powder vijiko 2 vya chakula
JINSI YA KUPIKA.
1.Vunja mayai uchanganye na sukari,uchukue mchapo(whisk) upige huo mchanganyiko bila kuachia mkono mpaka uvimbe uje juu,kisha tia mafuta endelea kupiga,na baadae tia maziwa, kisha endelea kama kwa dakika 3 kisha tia unga wa sembe na wangano ambao umeuchanganya na ile baking powder uchanganye vizuri kwa kutumia mwiko.
2.Weka mchanganyiko katika sufuria ambayo umeipaka mafuta kisha choma kwa oven au mkaa kama ni mkaa hakikisha moto ulishakolea.
3.Choma mpaka uwe na rang ya gold,uchome na kijiti kirefu ktk mkate, kama ushaiva kijiti kitatoka kisafi,hakina mnato,hapo ujue mkate wako tayari, utoe ktk sufuria acha upoe kisha ndio uukate,ENJOY kwa chai n.k.
NB:- pia kama huna maziwa unaweza kutumia tui zito la nazi badala ya maziwa
-mkate huu ni kama keki kabisa hivyo hautiwi hamira.
Bids
BID Stats : 0 Bids posted on this ad
Let’s Create Your Bid
Only registered user can post offer *
Ad Price
3,000